- 4,817 viewsDuration: 3:13Kinara wa DCP Rigathi Gachagua amempa ilani Rais William Ruto kuwa hana idadi toshelezi ya wapiga kura ya kumhakikishia muhula wa pili ofisini. Akizungumza katika Kaunti ya Kajiado, Gachagua amesema kuwa muungano wa upinzani utamshinda Ruto katika uchaguzi mkuu ujao. Amesema pia kuwa eneo la Mlima Kenya lenye uzito wa wapiga kura nchini tayari limeapa kutompigia kura Rais Ruto tena.