- 2,663 viewsDuration: 1:33Aliyekua naibu wa rais Rigathi Gachagua, ameonya kuwa eneo la Mlima Kenya liko kwenye hatari ya kusambaratika iwapo litamruhusu Rais William Ruto kuligawanya. Akizungumza wakati wa ibada ya kanisa katika Kaunti ya Kirinyaga, Gachagua aliwaonya wabunge wa Mlima Kenya dhidi ya kutumiwa kugawanya eneo hilo, akiongeza kuwa uhai wa kisiasa wa eneo hilo unategemea umoja wao. Kiongozi wa chama cha Wiper patriotic front, Kalonzo Musyoka, amewahakikishia wafuasi wa upinzani kwamba timu yao itamshinda Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027