Skip to main content
Skip to main content

Gachagua apinga uamuzi wa seneti mahakamani

  • | Citizen TV
    1,835 views
    Duration: 3:00
    Mawakili wa aliyekuwa Naibu Rais, Rigathi Gachagua, sasa wanaiomba Mahakama kubatilisha uamuzi wa Bunge la Seneti wa kumwondoa ofisini. Katika kesi hiyo iliyosikilizwa leo, mawakili wa Gachagua wanadai kuwa zoezi la kutafuta maoni ya wananchi kabla ya hoja hiyo kujadiliwa bungeni lilikiuka Katiba. Pia wanahoji kuwa zoezi hilo liliibua maswali kuhusu kwa nini kamati ya maseneta 11 haikubuniwa ili kumsikiliza Gachagua kabla ya uamuzi kuchukuliwa.