Gachagua atoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano baina ya mataifa ya mashariki ya Afrika

  • | KBC Video
    51 views

    Naibu rais Rigathi Gachagua ametoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano baina ya mataifa ya mashariki ya Afrika katika kushughulikia changamoto za usalama ili kuhimiza maendeleo. Naibu wa rais ambaye alifungua rasmi kongamano la usalama baina ya mataifa ya kanda ya Afrika mashariki huko Mombasa, aliongeza kuwa eneo hili bado linakabiliwa na tishio la uhalifu ukiwemo ulanguzi wa binadamu hasa watoto, tatizo la mihadarati, ufisadi, ulanguzi wa pesa miongoni mwa maovu mengine.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive