Gachagua awafokea viongozi wanaotoa matamshi ya kulipaka tope eneo la Mlima Kenya

  • | Citizen TV
    1,887 views

    Naibu Rais Rigathi Gachagua Amewafokea Baadhi Ya Viongozi Kutoka Eneo La Mlima Kenya Anaosema Wamezoea Kutoa Matamshi Yanayolipaka Tope Eneo Hilo. Gachagua Aliyezungumza Kaunti Ya Meru Hii Leo Saa Chache Baada Ya Ziara Ya Eneo La Nyanza Alikoonekana Kurushiwa Cheche Na Mbunge Wa Kikuyu Kimani Ichungwa’h Kwa Kuendeleza Siasa Za Kimaeneo Anasema Muda Umewadia Kwa Viongozi Kuficha Aibu Zao Wanapokuwa Hadaharani. Aidha Gachagua Anasema Hatokubali Tena Eneo La Kati Kutumika Kama Uwanja Wa Kueneza Chuki.