Gachagua: Serikali itawapa kipaumbele walioiunga mkono

  • | Citizen TV
    1,211 views

    Naibu rais Rigathi Gachagua ameendelea na matamshi yake kuhusu faida kwa waliounga mkono serikali ya Kenya Kwanza. Rigathi akisema serikali itawapa kipaumbele wale waliopigia kura Kenya Kwanza haswa katika nafasi za ajira na miradi ya maendeleo. Gachagua alikuwa akizumgumza katika kaunti ya Nandi ambapo aliandamana na afisa katika ofisi ya rais, Farouk Kibet na maafisa wengine serikalini kwa ibada kanisani na kisha kuchangisha pesa katika shule ya upili ya Kurgung.