Garshon Mutisya aliyeuwawa na polisi wakati wa maandamano amezikwa

  • | Citizen TV
    577 views

    Biwi la simanzi lilighubika kijiji cha Makutano viungani mwa mji wa Emali katika mazishi ya Garshon Mutisya, kijana aliyeuawa kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano ya tarehe 25 Juni. Familia, jamaa na marafiki waliohudhuria mazishi hayo wakiwashutumu maafisa wa polisi kwa kutumia silaha dhidi ya waandamanaji na serikali kwa kukosa kushughulikia maswala yanayoibuliwa. Viongozi wa kaunti hiyo, walikashifu agizo la Rais la waandamanaji kupigwa risasi ya Miguu huku wakitaka haki kwa familia zilizopoteza wapendwa wao. Marehemu akitajwa kama kijana aliyekuwa tegemeo katika familia yake.