Gavana aelezea hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali kuwanusuru wananchi

  • | VOA Swahili
    819 views
    Huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Meja Jenerali Peter Cirimwami ambaye pia ni Gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini siku ya Alhamisi ametembelea maeneo ambayo yanashambuliwa na waasi wa M23 hadi kwenye maeneo ya makazi ya raia yenye idadi kubwa ya watu. Makazi hayo yako mjini karibu mji wa Goma na eneo la Sake kiasi cha kilometa 25 magharibi ya mji mwa Goma. Gavana Cirimwani alifuatana na Kamati ya Usalama ya jimbo la Kivu Kaskazini. Meja Jenerali Cirimwami baadaye alitembelea kambi mbalimbali za wakimbizi zilizopo maeneo ambapo yanaendelea kukumbwa na mapigano. Ripoti hii maalum imeandaliwa na mwandishi wetu wa Goma Austere Malivika aliyefanya mahojiano maalum na Gavana Cirimwani ambaye ameelezea hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali kuwalinda wananchi na kuwahakikishia kuwa serikali yao itafanikiwa kurejesha utulivu. Endelea kusikiliza… #drc #goma #kivukaskazini #waasi #m23 #mejajenerali #PeterCirimwami #voa #voaswahili #rais #felixtshisekedi