Gavana Anne Waiguru aamuru baa zote zifungwe

  • | Citizen TV
    3,686 views

    Gavana wa Kirinyaga Ann Waiguru ameagiza kufungwa kwa baa zote katika kaunti ya Kirinyaga. Wakati wa ibada ya watu 17 waliofariki baada ya kunywa pombe haramu katika eneo la Mwea kaunti ya Kirinyaga, Waiguru, ambaye alifutilia mbali leseni zote za baa na vileo, pia amewapa notisi maafisa wa kaunti wanaosemekana kumiliki baa kaunti hiyo, waache biashara hiyo.