Gavana Arati na Mbunge Silvanus Osoro wako tayari kumaliza mgogoro wa kisiasa kati yao huko Kisii

  • | Citizen TV
    2,610 views

    Gavana wa Kaunti ya Kisii Simba Arati na Mpinzani wake Mbunge wa South Mugirango Silvanus Osoro wamesema kuwa wako tayari kufanya mashauriano na viongozi wakongwe katika kaunti ya Kisii ili kumaliza tofauti zao za kisiasa. Hata hivyo viongozi hao wawili bado wanalaumiana na kutaka kila mmoja abebe lawama zake kabla ya kikao hicho kuandaliwa. Viongozi hao wamekuwa wakizozana na kupelekea vurugu kuzuka katika maeneo tofauti kaunti ya Kisii.