Gavana Kiraitu Murungi ampigia debe Raila Odinga Meru

  • | Citizen TV
    5,275 views

    Gavana Wa Meru Kiraitu Murungi ameendelea kumpigia debe kinara wa Azimio One Kenya Raila Odinga akimtaja kuwa mkombozi wa watu wa jamii ya Wameru. Kiraitu aliyendamana na nduguye Raila, Oburu Odinga kwenye mkutano kaunti ya Meru amewahakikisha wakaazi kuwa matatizo yao ya jadi yatashughulikiwa endapo watampa kura ifikapo Agosti tarehe 9. Ameelezea imani kuwa Wameru wataunga mkono na kupigia kura Azimio zaidi kwenye uchaguzi wa mwezi ujao