Gavana Sakaja azindua hospitali ya macho ya mama Lucy

  • | K24 Video
    22 views

    Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja amezindua hospitali ya macho ya mama Lucy hii leo, inayolenga kutoa huduma muhimu za macho kwa wakaazi wa Nairobi na kwingineko. Ufunguzi wa kituo hicho unakwenda sambamba na takwimu za mpango mkakati wa kitaifa wa afya ya macho wa 2020, zinazoashiri kuwa asilimia 15.5 ya wakenya wanahitaji huduma bora za matibabu ya macho.