Gavana wa Kakamega Fernandes Barasa awaonya wakandarasi wazembe

  • | Citizen TV
    261 views

    Gavana wa kakamega Fernandes Barasa ametoa onyo kwa wanakandarasi wanaozembea kazini kwamba atawapiga kalamu. Alikuwa akizungumza katika soko la Sichirai eneo bunge la Lurambi ambalo limejengwa kwa muda murefu bila ya kukamilika. Soko la Sichirai lilitarajiwa kukamilika mwaka wa 2022 na bado halija fikia asilimia themanini ya ujenzi.