- 272 viewsDuration: 1:11Gavana wa Kaunti ya Baringo, Benjamin Cheboi, ametangaza kuwa hatatii mwaliko wa bunge la Seneti hadi mgogoro unaoendelea kati ya magavana na maseneta utakapotatuliwa. Kauli hii imekuja baada ya kutofika kwake mbele ya Kamati ya Seneti ya Hesabu za Umma, ambapo alitarajiwa kujibu maswali kuhusu ukaguzi wa hesabu na uwajibikaji wa kaunti.