Gavana wa Kaunti ya Samburu Lati Lelelit awarai wahudumu wa afya kutogoma

  • | Citizen TV
    144 views

    Huku wahudumu wa afya katika kaunti sita wakianza rasmi mgomo kufuatia kucheleweshwa kwa mishahara yao, Gavana wa Kaunti ya Samburu Lati Lelelit amewarai wahudumu wa afya kutogoma. Gavana Lati alifanya kikao na wahudumu wa afya katika hospitali ya rufaa ya Samburu na kuwataka kuwa na subira wakati huu ambapo kuna changamoto za kifedha nchini.