Gavana wa Kwale amulikwa kwa ubadhirifu

  • | KBC Video
    24 views

    Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani huenda akalazimika kutozwa shilingi milioni 2 baada ya kugunduliwa kutoa malipo yasiyo halali kwa baraza la magavana ili kugharamia kongamano la ugatuzi la mwaka 2023 lililoandaliwa katika kaunti ya Uasin Gishu. Serikali ya kaunti hiyo ilitoa mchango wa shilingi milioni 4 kwa jumla kwa ajili ya mwaka wa kifedha wa 2023/2024, shilingi milioni 2 zikitumika kugharamia kaunti ya Kilifi kushiriki katika kongamano pamoja na shilingi nyingine milioni 2 za ziada kwa ajili ya gharama ya ambayo tayari hushughulikiwa kwa mujibu wa sheria ya uhusiano baina ya serikali. Maseneta wamependekeza tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC kuhakikisha pesa hizo zimerejeshwa .

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive