- 54 viewsGavana wa Machakos Wavinya Ndeti ameanza zoezi la usambazaji wa mbegu kwa wakulima katika maeneobunge yote 8 katika kaunti nzima. Akizungumza wakati wa kuanza kwa usambazaji wa mbegu katika uwanja wa Kathaana katika kaunti ndogo ya Kangundo, Wavinya alisema kwamba serikali yake itahakikisha wakulima wanapata mbegu bora za mazao ya vyakula.