- 303 viewsGavana wa Makueni Mutula Kilonzo jr amemkosoa vikali waziri wa afya Aden Duale kuhusu matamshi yake ya hivi majuzi kuwa hawezi kufanyiwa lolote hata kama ngamia wanaotoka maeneo ya Garissa wataendelea kuharibu mimea ya wakaazi wa maeneo ya ukambani. Mutula ameyataja matamshi ya Duale kama yasiofaa na hususan wakati huu ambapo kuna msukosuko wa kiusalama katika eneo la Mwingi uliosababishwa na mzozo kati ya wafugaji wa ngamia na wakulima wa eneo la Mwingi.