Gavana wa Samburu atoa msaada wa elimu ya zaidi ya shilingi milioni 130

  • | Citizen TV
    115 views

    Gavana wa Samburu Lati Leleti, amesema serikali yake imeweka mikakati ya kukabiliana na udanganyifu uliokuwepo na kusababisha kufujwa Kwa fedha za umma kupitia karo ya wanafunzi. Gavana amemtaka waziri wa Elimu na maafisa wengine Katika serikali yake kupeleka hundi za karo katika vyuo vikuu,na taasisi mbali mbali za elimu ili kubaini kama kweli waliopokezwa ufadhili huo ni wanafunzi halisi wa vyuo na taasisi husika. Katika muongozo huo mpya kila mwanafunzi atafaidika na takribani shilingi elfu 15. Alisema hayo alipotangaza ufadhili wa shilingi milioni 134 kwa wanafunzi kutoka familia zisizojiweza.