'Gaza na ni kituo cha siri cha nguvu za wapiganaji wa Hamas katika eneo hilo'

  • | VOA Swahili
    388 views
    Mahandaki ya Hamas huko Gaza ndio lengo kuu la Israel wakati ikipanua mashambulizi yake ya ardhini kuingia eneo lenye msongamano wa watu katika kulipiza kisasi shambulizi la kushtukiza lililosababisha mauaji lililofanywa na kikundi cha Kiislam ndani huko kusini mwa Israel Oktoba 7. Mkuu wa zamani wa Ofisi ya Habari Jerusalem Stephen Farrell anaeleza: Gaza ni kituo cha Hamas, na kuna mtandao mkubwa wa mahandaki huko. Gaza na ni kituo cha siri cha nguvu za kijeshi katika eneo hilo. Hilo ndio eneo la Hamas kukimbilia kujificha, kuwaficha mateka, na kurusha roketi, kuhifadhi silaha, na ndio sababu mtandao huo ni muhimu sana kwa Israel. Hatua ya kwanza, imeharibu eneo la juu ya ardhi lililokuwa linaficha mahandaki hayo ili wapiganaji wa Hamas wasiwe na mahali pa kukimbilia. Hivi sasa, majeshi ya Israeli yanaingia chini ya ardhi ili kuweza kuwaokoa mateka, kuwaua au kuwakamata wapiganaji wa Hamas na kuwazuia au kuwasitisha wasiweze kamwe kufanya kitendo hiki tena. Nimekuwa katika baadhi ya haya mahandaki huko Gaza. Yale madogo ya kibiashara ni kiasi cha futi tatu hadi nne kwa upana. Mahandaki ya kijeshi ni yenye mfumo imara zaidi, yamejengwa kwa zege, na kina chake kikubwa. Itakuwa vigumu sana, sana, sana kabisa kwa Israel kuwatokomeza wapiganaji wa Hamas kutoka katika mtandao huo. #gaza #israel #palestine #reels #igreels #videography #voa #voaafrica #dagestan #russia