Genge la wezi lachipuka katika kaunti ya Kajiado

  • | Citizen TV
    327 views

    Wakazi wa mji wa Ilbissil, kaunti ya Kajiado, wanaishi kwa hofu kufuatia kuchipuka kwa magenge ya wezi ambayo yamekuwa yakiendeleza wizi katika mji huo. wezi hao sasa wameanza kuiba katika afisi za serikai ambapo walivamia afisi ya utoaji vitambulisho, ile ya DO na chifu katika mji huo na kuiba vifaa vya Kielektroniki. Tayari washukiwa wawili wametiwa mbaroni na wanaendelea kusaidia Polisi kwa uchunguzi.