Guinea-Bissau: Wanajeshi kutoka vikundi mbalimbali vya jeshi wakipambana

  • | VOA Swahili
    519 views
    Wanajeshi kutoka vikundi mbalimbali vya jeshi huko Guinea-Bissau wakipambana baada ya wanajeshi kuwaachia viongozi wawili wa serikali. Bissau: Mapigano yamezuka usiku kucha kati ya pande mbili hasimu za jeshi la Guinea-Bissau katika mji mkuu na kuendelea siku ya Ijumaa, Desemba 1, baada ya wanajeshi kutoka ulinzi wa taifa kumuachia huru waziri mmoja ambaye alikuwa akishikiliwa kwa kushukiwa kutumia vibaya fedha za umma. "Hali hivi sasa imedhibitiwa kikamilifu,” msemaji wa mnadhimu mkuu wa jeshi Captain Jorgito Biague aliiliambia shirika la habari la AFP. #guineabissau #umarosissocoembalo #suleimanseidi #antoniomonteiro