Hafla ya kitaifa ya kumuaga Rais mstaafu Benjamin Mkapa

  • | BBC Swahili
    Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ameongoza mamia ya watu katika hafla ya kitaifa ya kumuaga rais mstaafu wa taifa hilo Benjamin Mkapa ambaye aliaga dunia usiku wa kuamkia Ijumaa. Toka Jumapili mwili wa Marehemu Mkapa umekuwa ukiagwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Hii leo, ni zamu ya viongozi wakuu wa taifa hilo pamoja na wageni kutoka nje kuaga. Mzee Mkapa anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Lupaso, mkoani Mtwara kusini mwa Tanzania. #bbcswahili #Tanzania #Benjaminmkapa #Mkapa