Hafla ya maombi Kajiado

  • | Citizen TV
    553 views

    Maelfu ya wakaazi wa kaunti ya kajiado walijitokeza kwa hafla ya maombi kuwaombea na kutoa shukrani kwa wazee katika jamii. Wazee 300 waliofikisha umri wa miaka 70 wamejumuishwa kwenye hafla hii ambayo huandaliwa kila mwaka. Nyimbo za kitamaduni na densi za Kimaasai zilishamiri kwenye hafla hii iliyofikia kilele hii leo. Zaidi ya watu 2000 kutoka sehemu mbalimbali za jamii ya Maasai walifika kushiriki hafla hii ya maombi. Wakati wa hafla hii, wazee hawa pia huwabariki vijana huku waliofika wakifurahia dhifa na chakula cha kitamaduni