"Haipendezi katika mchakato wa ubunge ni watu wa familia za viongozi"

  • | BBC Swahili
    8,126 views
    Aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Cuba Humprey Polepole amekosoa utararitibu wa uchaguzi wa ndani wa chama chake cha CCM akidai kuwa chama hicho kina nafasi ndogo ya uongozi hivyo kila mmoja apewe nafasi ya kugombea tofauti na kuwa na wagombea wa aina moja kutoka familia za uongozi Polepole, aliyewahi kuwa msemaji wa chama tawala na kutetea masuala tata, kama kukiukwa kwa haki za binadamu na kukiukwa taratibu za uchaguzi wa mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020 ametoa kauli hiyo baada ya CCM kuwachuja watia nia ya ubunge katika uchaguzi wa Oktoba mwaka huu. - Hata hivyo hivi karibuni msemaji wa CCM Amos Makalla alisema kwamba mchakato wa kuwapata wagombea hao umefuata katiba na kanuni za CCM na mchakato wa kuwapata mgombea wa Urais na Makamu wa urais ulikamilika toka January #bbcswahili #tanzania #uchaguzi2025 Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw