- 287 viewsDuration: 3:12Huko Segera kaunti ya Laikipia, mlio wa kengele za shule ulikuwa nadra kusikika kwa miaka mingi, huku ukosefu wa usalama na umbali wa shule ukizuia watoto wengi kufika darasani. Leo, simulizi hiyo inabadilika polepole, huku shule ya misheni iliyoanzishwa zaidi ya muongo mmoja uliopita ikirekodi matokeo mazuri ya kitaaluma, kupanua fursa za elimu na kurejesha matumaini kwa familia nyingi.