Hali ya uwanja wa Bukhungu yaleta tumbo joto kwa waandalizi wa michezo ya sekondari Afrika Mashariki

  • | Citizen TV
    534 views

    Michezo ya shule za sekondari za Afrika Mashariki huenda ikalazimishwa kutafuta ukumbi mpya ikiwa uwanja wa Bukhungu huko Kakamega hautakamilika mwezi mmoja ujao. Shirikisho la michezo ya shule za sekondari za Afrika Mashariki limeelezea kusikitishwa kwao na hali ya uwanja kwa sasa kumbi zingine zilizotengwa kwa michezo hiyo Kakamega ziko katika hali nzuri, lakini uwanja wa Bukhungu ambao ni ukumbi mkuu wa mechi za kandanda una siku 30 tu kabla ya timu hiyo kufanya ukaguzi mwingine. Kumbi za Kakamega zitajaribiwa wakati wa mashindano ya kitaifa ya michezo za muhula wa pili ambayo itaanza tarehe 26 Julai. Serikali ya kaunti kupitia mtendaji mkuu wa michezo Jackline Masicha imeahidi kuwa uwanja huo utakuwa tayari kwa michezo ya shule ya kitaifa, na pia michezo ya Afrika Mashariki. Matukio hayo mawili yametofautiana kwa siku kumi tu.