Halima Mdee: Mimi ni CHADEMA ila sina tabia ya kususa

  • | BBC Swahili
    22,018 views
    Mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chama cha Demokrarasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania, Halima Mdee amesema atazungumzia hatma yake ya kisiasa baada ya Bunge la nchi hiyo kuvunjwa mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu, kwani kwa sasa bado hajafikia uamuzi. - Halima, aliyewahi kuwa mbunge wa kuchaguliwa wa Kawe jijini Dar es Salaam kwa miaka 10, ametoa tamko hilo wakati wa mahojiano maalumu na mwandishi wa BBC, Florian Kaijage huku akizungumzia kwa mara ya kwanza utaratibu uliomwingiza bungeni yeye na wenzake kumi na wanane mwaka 2020 na kuzua mgogoro yao na Chadema. - #bbcswahili #siasa #tanzania #chadema #uongozi Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw