Hatma ya wahudumu wa UHC haijulikani

  • | KBC Video
    6 views

    Baadhi ya wahudumu wa afya wanaohudumu chini ya mpango wa afya kwa wote-UHC wameridhia agizo la wizara ya afya la kuhamisha mfumo wa ulipaji wa mishahara yao hadi kwa serikali za kaunti kuanzia tarehe mosi mwezi ujao. Hatahivyo, wamesema uamuzi huo utaafikiwa tu iwapo shinikizo yao kuajiriwa kwa kandarasi ya kudumu itatimizwa. Haya yanajiri huku mwenyekiti wa kamati ya afya ya baraza la magavana Muthomi Njuki akipongeza agizo la wizara hiyo, akitoa wito wa kuhesabiwa kwa wahudumu hao wa afya, akidai huenda kuna wafanyakazi hewa elfu-3 miongoni mwa wafanyakazi wanaohudumu chini ya mpango wa UHC.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive