Hatua ya serikali ya kufunga maeneo ya kuuzia vileo kwenye maeneo ya kuishi

  • | K24 Video
    68 views

    Muungano wa vituo vya kurekebisha tabia humu nchini umeunga mkono hatua ya serikali kufunga maeneo ya kuuzia vileo kwenye maeneo ya kuishi ,na karibu na vyuo. Muungano huo unahofia kuongezeka kwa maduka ya pombe kutaongeza idadi ya waraibu ,wakati ambapo gharama ya huduma ya kubadilisha mienendo na kukabiliana na uraibu ni ya juu. Wameomba shirika la nakada kufanya majadiliano na serikali ya kitaifa ili kuongeza matibabu ya uraibu kwenye orodha ya huduma chini ya bima ya nhif .