'Hatuna mahali popote pa kulala'

  • | BBC Swahili
    1,821 views
    Idadi ya watu waliokimbia makazi yao kutokana na mafuriko nchini Somalia imeongezeka hadi 100,000 katika kipindi cha wiki moja tu. Mvua kubwa iliyonyesha mwezi Oktoba imesababisha vifo vya zaidi ya watu 100 katika eneo la Pembe ya Afrika. Miji yote imeathirika, pia katika maeneo ya Kenya na Ethiopia. Maeneo yaliyoathiriwa yalikuwa hayajapata auheni kutokana na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea eneo hilo katika miongo 4. Huku mvua nyingi zikitabiriwa, watu wanatelekeza nyumba zao na kuhamia maeneo makavu huku serikali na mashirika ya misaada yakijaribu kuwafikia walioathirika. #bbcswahili #ukame #ethiopia Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw