"Hatuna 'tiger' Kenya," Rigathi Gachagua ajitetea kutokana na matamshi yake akiwa nchini Colombia

  • | Citizen TV
    9,831 views

    Naibu rais Rigathi Gachagua amejitetea kutokana na matamshi yake akiwa nchini Colombia kuhusu kuwepo kwa simba marara nchini Kenya. Akizungumza katika hafla ya shirika la msalaba mwekundu jijini Nairobi jana jioni, naibu rais alijikosoa akisema kuwa alimaanisha chui na wala sio simba marara. Gachagua aidha alitumia fursa hiyo kuwataka watalii pia kufika kwenye mbuga ya wanyama ya Nairobi kufurahia wanyama pori