Skip to main content
Skip to main content

Herice Mukele: Mwanamke anayeota ndevu kwa wingi kama wanaume

  • | BBC Swahili
    5,527 views
    Duration: 8:00
    Herice Mukele mkazi wa Muleba mkoani Kagera nchini Tanzania anasema watu wengi wamekuwa wakimnyooshea vidole na kudai kuwa anajinsia mbili kutokana na hali aliyonayo ya kuota ndevu kwa wingi sawa na wanaume. Akiwa na miaka 16 ndevu zilianza kutoka moja moja jambo lilompa wasiwasi mkubwa lakini Bibi yake alimwambia asinyoe kwani hayo ni mabadiliko ya kawaida tu ya mwili Kwa sasa amejizolea umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kwa namna anavyozitunza ndevu zake na mitindo wake wa kunyoa jambo linalovutia watu wengi Kwa mujibu wa Daktari Selestine Mpili toka hospitali ya huduma za kibingwa ya Mdinova ya Jijini Dar es salaam anasema kitaalamu hali hii inasababishwa na mvurugiko wa homoni na inaweza kurekebishwa kwa kupata matibabu sahihi. Mwandishi wa BBC Eagan Salla na taarifa zaidi……. #tanzania #afya #homoni Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw