Hofu ya janga la kibinadamu yaongezeka Gaza
Umoja wa mataifa Jumanne ulionya dhidi ya mashambulizi ya ardhini huko Rafah katika Ukanda wa Gaza, ukisema mashambulizi hayo yanaweza kusababisha mauaji makubwa katika eneo hilo la kusini mwa Palestina ambako zaidi ya watu milioni 1 wanaishi.
Israel imesema inataka kuwaondoa wanamgambo wa Hamas kwenye maficho yao huko Rafah na kuokoa mateka wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas, na inaandaa mipango ya kuwaondoa raia wa Palestina waliokwama huko.
“Operesheni za kijeshi huko Rafah zinaweza kusababisha mauaji makubwa huko Gaza. Zinaweza pia kukwamisha shughuli za kutoa misaada ya kibinadamu ambazo tayari zilikuwa zimedhoofika,” alisema mkuu wa misaada ya kibinadamu kwenye Umoja wa mataifa Martin Griffiths.
Alisema katika taarifa kwamba “Jumuia ya kimataifa imekuwa ikionya dhidi ya athari mbaya za mashambulizi ya ardhini huko Rafah, na serikali ya Israel haiwezi kuendelea kupuuza wito wa Jumuiya ya Kimataifa.
Mazungumzo yanayojumuisha Marekani, Misri, Israel na Qatar kuhusu sitisho la mapigano Gaza yalimalizika Jumanne bila kupiga hatua yoyote huku shinikizo likiongezeka kwa Israel kuachana na mpango wake wa kuishambulia Rafah.
Wakati huo huo Al-Tikeye taasisi ya hisani yenye makao yake Rafah inaendelea kuwalisha Wapalestina wengi wao watoto na wanawake wanaokabiliwa na njaa waliokoseshwa makazi katika mji ulioko upande wa kusini wa Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa wizara ya afya Gaza inayoendeshwa na Hamas mashambulizi ya angani na ardhini yanayofanywa na Israel yameuwa watu zaidi ya 28,000 na kujeruhi zaidi ya wengine 65,000 katika eneo finyu la Gaza.
Mashambulizi haya yalianza Oktoba 7 kufuatia mauaji ya Oktoba 7 huko kusini mwa Israel, yaliofanywa na wanamgambo kutoka Gaza waliouwa takriban watu 1,200 na kuwateka watu 250. - AP
#Haifa #waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu
#Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #wahouthi #marekani #uingereza #shambulizi #dhamar #yemen #iran
5 Jul 2025
- ODM was responding to The Standard Media's 'Raila's Turf Rebels' article.
5 Jul 2025
- The closure is set to affect major transport activities in the heart of Kenya's capital.
5 Jul 2025
- The incident happened on Friday evening, causing tension.
5 Jul 2025
- The Orange Democratic Movement (ODM) has slammed media reports which claimed that the party leader, Raila Odinga, is losing popularity in his backyard of Nyanza due to the events that unfolded during the burial of late teacher Albert Ojwang' at Kakoth…
5 Jul 2025
- The Judicial Service Commission (JSC) has strongly condemned what it terms as excessive use of force by police officers during the re-arrest of youth politician Peter Kinyanjui, alias Kawanjiru within the Ruiru Law Courts, saying the actions undermine…
5 Jul 2025
- Former Deputy President Rigathi Gachagua has launched scathing accusations against President William Ruto, claiming the Head of State is systematically persecuting the Mt. Kenya community.
5 Jul 2025
- Royal Media Services was on Friday night recognized as one of the top community promoters of road safety in Kenya.
5 Jul 2025
- National chair Gladys Wanga reaffirmed Raila’s status as a towering national figure.
5 Jul 2025
- The suspects are currently in custody and will be arraigned once investigations are completed.
5 Jul 2025
- They will join other reporters from around the world after passing rigorous recruitment processes.
5 Jul 2025
- ODM was responding to The Standard Media's 'Raila's Turf Rebels' article.
5 Jul 2025
- Muslim religious leaders in Mombasa are now urging President William Ruto to build a mosque within the State House, following his recent admission that a church has been constructed on the grounds.
5 Jul 2025
- Bill seeks to remove time limit condition for application for citizenship by stateless persons.