Hofu ya usalama yazuka Mombasa kufuatia mauaji

  • | Citizen TV
    3,003 views

    Familia moja mjini Mombasa inalilia haki baada ya jamaa yao kupigwa risasi na wahalifu katika mtaa wa Karama eneo bunge la Nyali. Judy Ndunda kamene aliyekuwa mfanyabiashara wa duka la mpesa aliuwawa na genge hilo mita chache karibu na nyumba yake. Genge hilo linadaiwa kutoweka na pesa na simu na kufikia sasa hakuna mshukiwa aliyekamatwa.