Hofu yatanda DRC baada ya mauaji ya zaidi ya watu 40 kanisani.

  • | BBC Swahili
    408 views
    Umoja wa mataifa na jeshi la taifa hilo yanasema kuwa zaidi ya watu arobaini, wakiwemo watoto tisa waliuawa katika shambulio la kundi la waasi la Allied Democratic Forces au ADF wenye uhusiano na kundi la Islamic State siku ya Jumapili. Waliofariki ni waumini wa kikristo waliokuwa ibadani walipovamiwa usiku wa jumamosi.