Hofu yatanda katika mtaa wa Mawanga baada ya mauaji ya kutatanisha ya wanawake watatu

  • | KTN News
    592 views

    Hofu imetanda katika mtaa wa Mawanga eneo bunge la Bahati kaunti ya Nakuru baada ya mauaji ya kutatanisha ya wanawake wasiopungua watatu katika kipindi cha juma moja. Mauaji hayo ambayo yanafanyika mchana peupe yanaonekana kufwata mpangilio sawia huku wauwaji wakiwalenga wanawake waliobaki nyumbani pekee yao. Katika visa hivyo, waathiriwa wananajisiwa, baadaye kunyongwa ama kupigwa hadi kufa kisha miili yao inateketezwa. Wanawake sasa wanalazimika kukaa mbali na makwao mchana kutwa kwa hofu ya kuviziwa na wauwaji hao.