Hoja ya kumtimua Gachagua kuwasilishwa bungeni wiki ijayo

  • | Citizen TV
    7,084 views

    Wabunge Wa Bunge La Kitaifa Sasa Wanajiandaa Kuwasilisha Hoja Ya Kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua Ofisini Wiki Ijayo, Baadhi Ya Viongozi Bungeni Wakisema Tayari Wamekusanya Zaidi Ya Saini 270 Kuanzisha Mchakato Huo. Kama Anavyoarifu Mwanahabari Wetu Wa Masuala Ya Siasa Emmanuel Too, Wabunge Hao Hawajaafikiana Ni Mbunge Yupi Atakayewasilisha Hoja Hiyo, Wakisema Mchakato Huo Unaongozwa Kisiri Ili Kufunga Mianya Yote Ya Mchakato Huo Kubatilishwa Mahakamani.