| Hongera Harambee Stars |

  • | Citizen TV
    611 views

    Hongereni sana kwa kuheshimisha taifa, hongereni sana kwa kuregesha matumaini ya soka nchini. Hakuna aliyejua itakuwa vile. Na vile ilivyokuwa kuwa ilikuwa fahari ya taifa. Kwa muktadha wa mashindano sisi si washindi lakini kwa uhalisia wa kilichojiri sisi ni washindi tena wakubwa. Si siri japo kwa mukhtasari lakini hatutakosekana kwa historia ya CHAN 2024, sio tu kama nchi moja wapo iliyoandaa, sio tu kwa kufika hatua ya robo fainali tukiwa tunashiriki kwa mara ya kwanza, sio tu kwa kupata ushindi dhidi ya nchi mbili bora Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo na Morocco ambao wote ni washindi mara mbili bali kwa kuonesha maana na thamani ya soka nchini kuanzia kwa rais, wizara , shirikisho, mkufunzi na kikikosi chake hadi kwa mashabiki