Hospitali 12 zilizobakia zinazotoa huduma Ukanda wa Gaza ziko mashakani

  • | VOA Swahili
    254 views
    Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema Idadi ya hospitali zinazofanya kazi katika ukanda wa Gaza imepungua kutoka 36 hadi 18 tangu kuzuka kwa mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa hamas Octoba 7. Kwa mujibu wa WHO hospitali 12 zinazofanya kazi katika ukanda wa Gaza ndio zinatumika kama muhimili wa afya kwenye ukanda huo. Ikizingatiwa kwamba mashambulizi ya jeshi la ardhini la Israel kusini mwa Gaza yanaweza kusababisha maelfu ya wakazi kukosa huduma za afya, na hivyo WHO imetoa wito kwa Israel kulinda raia na miundombinu. Jumanne wagonjwa waliojeruhiwa walikuwa wanamininika katika hospitali ya Nasser moja wapo kati ya hospitali kubwa katika ukanda wa Gaza na kusababisha kituo hicho cha afya kuelekea kwenye ukingo wa kusitisha kazi zake. Jumatatu WHO ilisema katika taarifa yake kwamba wakati raia zaidi kusini mwa Gaza bado wanapata tahadhari ya kuondoka haraka na wanalazimishwa kuondoka, watu wengi wanakusanyika pamoja katika eneo dogo , wakati hospitali zilizobaki katika eneo zinafanya kazi kukiwa na upungufu wa mafuta, madawa, chakula maji na wafanyakazi wa afya. - Reuters #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #hospitali #Nasser #wagonjwa #madawa