Hospitali na mashirika waandaa matibabu bila malipo kwa wakazi wa Manga, Kitutu Masaba

  • | Citizen TV
    216 views

    Hospitali ya Equity Afya ikishirikiana na wakfu wa Clive Ogwora pamoja na hospitali ya New Hope inaendesha mradi wa matibabu bila malipo kwa wenyeji wa kaunti ndogo ya Manga eneo bunge la Kitutu Masaba, ili kuwasaidia wenyeji wasioweza kumudu gharama ya matibabu wanayohitaji. Wenyeji wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kwenye hafla hizo ambapo watapimwa dalili za magonjwa mbalimbali, mara hii wakizingatia kupima magonjwa kama shinikizo la damu na kisukari kabla ya kutoa dawa bila malipo. Tunaungana naye Duncan Bundi kutoka hospitali ya New Hope kule Gesure