Hospitali Niger zakabiliana na hali ngumu baada ya mapinduzi

  • | BBC Swahili
    1,017 views
    Imepita miezi miwili tangu mapinduzi ya Niger kufanyika. Wakati viongozi wa kijeshi walipomuondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum na kuweka serikali yao wenyewe, Ecowas iliiwekea nchi hiyo vikwazo, kufunga mipaka na kukata umeme. Matokeo yake - sekta ya afya Niger ipo katika wakati mgumu. Mwandishi wa BBC alisafiri hadi mji wa Gaya wa Niger, karibu na mpaka wa Benin na Nigeria, ili kujua jinsi hospitali, madaktari na wagonjwa wanavyokabiliana na hali hiyo #bbcswahili #niger #nigeria Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw