Hospitali nyingi za kaunti za Pwani zakumbwa na uhaba wa damu

  • | Citizen TV
    208 views

    Pwani ya Kenya inakumbwa na uhaba wa damu tatizo ambalo linadaiwa kuchangiwa na ulaji wa vyakula vya Waswahili kama vile Biriani, Pilau na Viazi Karai. Baadhi ya wakazi wamekuwa wakitaabika wanapohitaji damu na kulazimika kutafuta usaidizi kutoka kwa marafiki na familia. Na kama anavyoarifu Francis Mtalaki kituo cha kutoa na kuhifadhi damu kimedai kuwa mila na itikadi potovu pia zimechangia kuwepo kwa changamoto hii.