Hospitali ya Indonesia iliyoko Gaza imefungwa huku takriban wagonjwa 45 awakihitaji upasuaji

  • | VOA Swahili
    173 views
    Hospitali ya Indonesia iliyoko Gaza imefungwa huku takriban wagonjwa 45 awakihitaji upasuaji wa haraka wameachwa katika eneo la mapokezi, mkuu wa hospitali hiyo Atef al-Kahlout aliambia Al Jazeera . Hapo awali, hospitali hiyo ilionekana ikiwa imejaa watu waliojeruhiwa sakafuni, huku wahudumu wa afya wakimfanyia mgonjwa upasuaji wakitumia mwanga wa tochi kutokana na kukatika kwa umeme. Daktari katika hospitali hiyo, Yasmeen Abu Seif alisema kituo hicho kimeachwa bila vifaa, hakuna madaktari na uwezo wa kutibu majeruhi wanaoletwa.