Hospitali ya Mama Lucy Kibaki yajipata mashakani

  • | Citizen TV
    7,145 views

    Serikali ya kaunti ya Nairobi imefanya mabadiliko kwenye bodi ya usimamizi ya hopsitali ya Mama Lucy, saa chacha baada ya video ya mwanamke mja mzito kuonekana akitapatapa kwenye hospitali hiyo. Mageuzi haya yakijiri huku hisia mseto zikiendelea kuhusiana na tukio hilo ambapo mama huyo baadaye alimpoteza mwanawe kabla ya kujifungua.