Hospitali za kaunti ya Nyandarua zapokea shehena ya dawa za ksh.17.5M

  • | Citizen TV
    443 views

    Serikari ya kaunti ya Nyandarua imepokea na kusambaza dawa za matibabu za takriban shilingi milioni 17.5. Shehena hiyo ya dawa inatarajiwa kusambazwa katika vituo vyote vya afya 78 vilivyoko kaunti hiyo. Akihutubu wakati wa hafla ya usambazanji wa dawa hizo akiwa katika hospitali ya Engineer, iliyoko kaunti ndogo ya Kinangop, Gavana Moses Kiarie Badilisha amendokeza kwamba kwa muda wa siku kumi zijazo, serikari yake itapokea shehena nyingine ya dawa kama hizo za shilingi milioni kumi.