Huduma nyingi muhimu zimekatizwa katika eneo la Wajir Kaskazini

  • | Citizen TV
    5,434 views

    Jioni ya leo, janga kubwa linakodolea macho kaunti ya Wajir Kaskazini Mashariki ambako huenda wakati wowote wakaazi wakakosa kabisa chakula, bidhaa za mafuta na hata huduma nyingine muhimu kutokana na athari za mafuriko. Hii ni baada ya mvua kubwa inayonyesha kuharibu barabara kuu inayoingia na kutoka kaunti hiyo. Wanaoishi maeneo mbali ya mji wa wajir wako katika hatari zaidi kwani usafiri umekwama. Mwanahabari wetu AYUB ABDIKADIr yuko Wajir na hii hapa taarifa yake iliyoandaliwa Na Mashirima Kapombe.