- 1,903 viewsDuration: 2:11Hatma ya wanafunzi zaidi ya10,000 huko Mombasa imesalia katika njia panda baada ya kufukuzwa shuleni kwa kukosa kulipa karo katika shule za kibinafsi. Kulingana na muungano wa shule za kibinafsi kaunti ya Mombasa, serikali ya kaunti iliahidi kulipa zaidi ya shilingi milioni 40 mwaka mmoja uliopita ili kugharamia baadhi ya karo za wanafunzi Hao na wamekuwa wakipokea shutma kutoka kwa wazazi wanaodai risiti za malipo hayo. Kulingana na waziri wa elimu kaunti ya Mombasa Mbwarali Kame fedha hizo zimechelewa kulipwa kutokana na kucheleweshwa kupitishwa kwa bajeti ya ziada katika bunge la kaunti na kutaka wazazi kuwahamisha watoto hao katika shule za umma.