Hussein Abdille na Mohamed Abdi Ali wana hatia ya ugaidi Dusit

  • | Citizen TV
    1,764 views

    Mahakama imewapata na hatia washukiwa wawili wa shambulizi la kigaidi lilliotokea katika hoteli ya Dusit hapa Nairobi mwaka 2019. Hussein Mohamed Abdille Ali na Mohamed Abdi Ali, wamepatikana na hatia ya makosa yote 21 ya ugaidi, kufuatia idadi sawa ya watu waliouawa kwenye shamblizi hilo. Jaji Diana Kavedza akisema wawili hao walihusika kupanga na kutekeleza shambulizi hilo, ambapo mmoja wa magaidi hao alijilipua.