- 3,151 viewsDuration: 2:07Kwa miaka 20 Susan Nagi amekuwa akipambana na maambukizi adimu katika njia ya juu ya upumuaji yanayosababishwa na ugonjwa unaoitwa rhinoscleroma. Ugonjwa huo, ambao umeenea kutoka puani hadi machoni, umesababisha macho yake kuvimba kwa kiasi kikubwa, hali inayomfanya akumbane na unyanyapaa kwa jamii. Mbali na kuathiri afya yake ya mwili, ugonjwa huo pia ulimnyima nafasi ya kuendelea na masomo yake. Hata hivyo, Susan anaendelea kupambana kwa moyo wa uthabiti na matumaini, akijikubali alivyo na kusonga mbele na maisha yake #bbcswahili #Afya #afyayamacho Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw